Kuhusu Sisi

Tunaamini stori na malengo yetu kwenye biashara itakua moja ya sababu ya kukufanya uwe chachu ya mabadiliko kwenye maisha ya uwapendao.

From CO-Founder
Lengo letu kama kampuni ni kuhakikisha nguo za ndani zinapatikana kiurahisi kwenye jamii zetu za Kitanzania. Tunataka kutengeneza mazingira kila mwananchi awe na uwezo wa kununua underwear mahali popote kwa muda wowote.
AGNES HENERICO
CEO
Social Media
From CO-Founder
Nguo ya ndani nzuri inakupa confidence popote pale. Pia huongeza upendo baina ya wapendanao. Robians malengo yetu ni kukuza confidence na upendo kupitia Nguo za ndani zenye viwango.
Dr. ansbert mutashobya
Director
Social Media
Our Story
Kutengeneza na kuuza nguo za ndani zenye ubora na muonekano mzuri kwa binti, kijana, mama, na baba wa kiafrika.

Ni furaha sana kuihudumia jamii, ni furaha sana pale unapomhudumia mteja na kusema nashukuru sana kwa huduma – mke wangu au mume wangu au wanangu wamefurahia sana nguo ulizotuuzia.

Watu wengi wanasahau kubadilisha nguo za ndani, aanazivaa mpaka zinabadilika rangi na zinatoboka kwasbabu wakizivaa hamna anayewaona, wanasahau kujali afya zao. Nguo za ndani hukuza upendo na huleta kujiamini popote pale.

Mnamo mwaka 2019, mimi na mume wangu mpenzi Dr. Ansbert tuliamua kuwa chachu ya faida hizo kwa kuhakikisha tunatoa elimu ya kutosha kwa jamii juu ya faida za kubadilisha nguo za ndani mara kwa mara ili kujiweka maridadi na salama kiafya.

Aina Zote za Underwear

Robians Inajumuisha brands za aina nyingi ikiwemo Calvin Klein, Puma, 99v, na mengineyo.

Material ya Cotton Pekee

Nguo zetu zote zimetegenezwa na material ya cotton, kukufanya ujisikie fresh muda wote.

Afya Yako Kwanza

Tunafundisha jamii na wateja wetu kwenye masaula nyeti yanayohusiana na nguo za ndani.

Follow Us

Shopping Cart